TANZANIA YASHIRIKI MJADALA KUHUSU MATUMIZI YA AKILI MNEMBA KATIKA KUKUZA USIMAMIZI WA UCHUMI WA KIKANDA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameshiriki katika Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichojadili fursa na changamoto za matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika usimamizi wa uchumi jumla kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington DC, Marekani.
MEFMI ni taasisi ya kikanda inayolenga kujenga uwezo wa nchi wanachama katika usimamizi wa sera za uchumi jumla, masuala ya fedha, usimamizi wa madeni, pamoja na takwimu za kiuchumi.