TANZANIA YAPONGEZWA MATUMIZI YA VIWANGO VYA KIMATAIFA VYA UHASIBU WA SEKTA YA UMMA

Tanzania imepongezwa kwa kuwa miongoni mwa nchi kinara barani Afrika kutumia viwango vya kimataifa vya Uhasibu wa Sekta ya Umma (IPSAS), hatua iliyochangia kuweka uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma. Pongezi hizo zimetolewa mjini Accra, Ghana na Mshauri wa masuala ya matumizi ya viwango vya kimataifa vya uhasibu kutoka Zimbabwe, Bw. Amon Dhlimayo, wakati akitoa mada kuhusu matumizi ya viwango hivyo wakati Mkutano wa Tatu wa Wahasibu wa Serikali Barani Afrika (African Association of Accountants General Meeting (AAAG), unaofanyika nchini humo.