TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI MZURI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

Washirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan katika maeneo ya ukuaji wa uchumi, maendeleo ya rasilimali watu, mifumo ya chakula na miundombinu. Pongezi hizo zimetolewa jijini Dodoma katika Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati Ngazi ya Wataalamu kati ya Serikali (Makatibu Wakuu SMT na SMZ) na Washirika wa Maendeleo (Heads of Development Cooperation) ambayo yanalenga kujadili mbinu za kuongeza ustahimilivu wa kiuchumi na maendeleo jumuishi katika kipindi cha mabadiliko na changamoto za kiuchumia katika kipindi kisichotabirika.