TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. TRIL 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND

Tanzania na Global Fund zimesaini Mikataba minne ya misaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 606.9 (sawa na zaidi ya sh. trilioni 1.4) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini. Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison.