TANZANIA YANUFAIKA NA MIRADI YA UMEME NA MAWASILIANO KUPITIA EXIM BANK YA CHINA

Tanzania inaendelea kunufaika na miradi mikubwa ya mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa kupitia Benki ya Exim ya China ikiwa ni pamoja na Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme ya Kilovolti (kV) 400 Kaskazini-Mashariki (Dar es Salaam–Arusha) na mradi Upanuzi wa Mawasiliano ya Mtandao wa Simu Vijijini (Awamu ya Kwanza). Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) wakati wa mkutano na ujumbe wa Benki ya Exim ya China ulioongozwa na Naibu Meneja Mkuu wa Benki hiyo, Bi. Liu Fang.