TANZANIA YANG’ARA UUNGANISHAJI MFUMO WA MUSE NA CS- MERIDIAN
Tanzania imefanikiwa kuwa nchi ya kwanza kuunganisha Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) kwa nchi za Afrika uliotambuliwa na Jumuiya ya Madola na kuifanya kuwa kitovu cha mafunzo ya Mifumo hiyo.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, alipokuwa akifungua mafunzo kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya waliokuja nchini kujifunza namna Mifumo hiyo inavyofanya kazi.