TANZANIA YAJIPANGA KUWA GHALA LA CHAKULA DUNIANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ametoa wito kwa Wadau wa Maendeleo kushirikiana na Tanzania kupanga mikakati itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuboresha mifumo yake ya uzalishaji na kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula na kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula duniani. Dkt. Mwamba ametoa wito huo jijini Dar es Salam wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo ngazi ya Wataalam uliowashirikisha wadau wa maendeleo wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Asasi zisizo za Kiserikali (AZAKI), na Viongozi waandamizi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.