TANZANIA YAISHUKURU TRADEMARK AFRICA

Tanzania imeishukuru Taasisi ya Trademark Afrika (TMA) kwa mchango wao katika kuboresha mifumo mbalimbali inayochangia kuimarika kwa mazingira ya biashara uwekezaji nchini. Shukrani hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa inayosimamia utekelezaji wa miradi ya TMA nchini (National Oversight Committee -NOC), Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa NOC, Bodi ya Wakurugenzi wa TMA na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA).