TANZANIA YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI BINAFSI KATIKA NISHATI, YALENGA SOKO LA UMEME AFRIKA
Serikali ya Tanzania imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha Sekta ya Nishati kwa kushirikisha sekta binafsi katika uzalishaji na usambazaji wa umeme, huku ikiimarisha uwekezaji wa ndani katika miradi mikubwa ya nishati na kuandaa miundombinu ya kuuza umeme katika nchi jirani za Afrika Mashariki na maeneo mengine ya Afrika.
Dhamira hiyo imeelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, katika jopo la majadiliano kuhusu maendeleo ya Sekta ya Nishati, lililofanyika kama sehemu ya Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), uliofanyika mjini Cotonou, Jamhuri ya Benin.
