TANZANIA YAELEZEA UMUHIMU WA USHIRIKIANO NA MCDF KATIKA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania inahimiza umuhimu wa ushirikiano wake na Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Miundombinu (MCDF) katika kuimarisha miradi ya kimkakati na kuchochea maendeleo endelevu nchini. Mhe. Balozi amesema hayo wakati akihutubia katika kikao cha Mfuko huo kilichowashirikisha Mawaziri wa Fedha ambao ni Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB), kilichofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Magavana wa Benki hiyo, jijini Doha, nchini Qatar.