TANZANIA YAELEZA MAFANIKIO YA KIUCHUMI, USHIRIKIANO NA TAASISI ZA KIMATAIFA.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa uhusiano kati ya Tanzania na taasisi za fedha za kimataifa, ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), umeendelea kuimarika huku uchumi wa nchi ukionesha ukuaji wa kuridhisha.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo (12.10.2026) alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Ndiame Diop, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia inayofanyika Jijini Bangkok nchini Thailand.
