TANZANIA, UNDP KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA AJIRA KWA VIJANA NA UWEKEZAJI.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika kukabiliana na changamoto za ajira kwa vijana, kuendeleza elimu, kuvutia uwekezaji na kukuza sekta binafsi ili kuharakisha maendeleo ya uchumi wa nchi.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la UNDP Duniani ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ubelgiji, Bw. Alexander De Croo, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, jijini Bangkok, nchini Thailand.
