TANZANIA NA UJERUMANI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani zimehitimisha majadiliano ya ushirikiano wa maendeleo kwa kusaini Hati ya Makubaliano itakayoongoza ushirikiano wa nchi hizo mbili katika miaka ijayo. Majadiliano hayo yamefanyika tarehe 18 na 19 Novemba 2026, jijini Berlin, Ujerumani. Hati hiyo imesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, na Bi. Christine Toetzke, Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Ushirikiano wa nchi hizo mbili katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ), kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani.