TANZANIA NA UJERUMANI ZAJADILIANA USHIRIKIANO WA MAENDELEO

Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (Kushoto) pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Ujerumani wakiwa katika majadiliano ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Serikali hizo, ambapo Serikali ya Ujerumani imewasilisha makadirio ya bajeti ya msaada utakaotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini katika Sekta yza Maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Majadiliano hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.