TANZANIA NA UJERUMANI ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA MAENDELEO KWA WANANCHI NA UCHUMI.
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani zimeanza mazungumzo ya pande mbili kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa maendeleo, hususan katika miradi yenye matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi na Uchumi wa Taifa.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha Mtumba, jijini Dodoma, yalijikita katika maeneo mbalimbali ya kimkakati, yakiwemo maji na usafi wa mazingira, afya, nishati, matumizi endelevu ya rasilimali za asili na uhifadhi wa mazingira, upatikanaji wa haki, usimamizi bora wa fedha za umma pamoja na usawa wa kijinsia.
