TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania na Norway zinajivunia uhusiano imara wa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, uliochangia maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali. Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadiliana namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo.