TANZANIA NA MAREKANI KUSHIRIKIANA KIBIASHARA KUPITIA SEKTA BINAFSI
SERIKALI imesema imefungua milango ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Marekani kupitia Sekta Binafsi ili kuchochea biashara kupitia uwekezaji ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo kati ya Marais wa nchi hizo mbili yaliyofanyika hivi karibuni mjini Washington DC.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, walipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago.