TANZANIA NA JAPAN YASAINI MIKATABA YA MIKOPO YENYE MASHARTI NAFUU
Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), zimesaini mikataba mitatu ya mkopo wenye masharti nafuu na msaada, yenye thamani ya Yen bilioni 10.15, sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 174.9, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ununuzi wa pemebejeo za kilimo pamoja na kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).