TANZANIA NA INDONESIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA MAENDELEO KATIKA KILIMO NA NISHATI

Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo na nishati kwa faida ya nchi hizo mbili. Hayo yamebainishwa jijini Dodoma, baada ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omary (Mb), kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Tri Yogo Jatmiko Avetisyan. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Balozi Omar, ameishukuru Serikali ya Indonesia kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia sekta mbalimbali za uchumi wa Tanzania ikiwemo sekta za madini, kilimo na mifugo tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1964.