TANZANIA NA INDIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA 2050
Serikali ya Tanzania na India zimekubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey, aliyefika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha. jijini Dar es Salaam kujitambulisha.
