TANZANIA NA CZECH MBIONI KUONDOA UTOZAJI WA KODI MARA MBILI

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zimekamilisha majadiliano ya Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili yatakayowezesha wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizi mbili kutozwa kodi katika mapato yao katika nchi moja badala ya kila nchi kutoza kodi ya mapato. Majadiliano hayo ambayo yamefanyika katika duru ya tatu yalikutanisha pande hizo mbili Tanzania ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya na Serikali ya Czech ikiongozwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Masuala ya Kodi Kimataifa wa Wizara ya Fedha ya Czech, Bw. Václav Zíka, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.