TANZANIA NA BENKI YA EXIM YA UTURUKI WAJADILI UFADHILI WA RELI YA SGR NA UKUAJI WA BIASHARA

Serikali ya Tanzania iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Benki ya Exim ya Uturuki ili kupata ufadhili wa dola za Marekani milioni 280 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande cha tatu na cha nne cha mradi wa reli ya kisasa (SGR). Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Antalya nchini Uturuki, kando ya Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP31, kati ya ujumbe wa Tanzania ukiogozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar na Ujumbe wa Benki ya Exim ya Uturuki ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Ali Guney.