TANZANIA NA BENKI YA DUNIA ZAWEKA MKAKATI WA PAMOJA KUCHOCHEA MAGEUZI YA UCHUMI NA KUTENGENEZA AJIRA.

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na viongozi wa Benki ya Dunia jijini Bangkok, Thailand, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayofanyika nchini humo, kujadili mikakati ya kuharakisha maendeleo ya uchumi wa nchi, hususan katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu, uandaaji wa ajira na uhamasishaji wa uwekezaji wa sekta binafsi. Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Balozi Omar amesisitiza umuhimu wa kuelekeza jitihada za maendeleo kutoka katika kupima mafanikio kwa viashiria vya ukuaji wa uchumi pekee, badala yake izingatie matokeo halisi yanayogusa maisha ya wananchi, ikiwemo kuongeza uzalishaji, kupanua fursa za ajira na kuinua kipato.