TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA TATHIMINI WA BENKI YA DUNIA (IDA 20-MTR)

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Medium Term Review) utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukizishirikisha wajumbe zaidi ya 2590 kutoka matafaifa takribani 100 duniani. Hayo yamebainishwa mjini Marrakech, nchini Morocco, wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum, alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia dirisha la IDA (International Development Association), Bw. Akihiko Nishio, kando ya Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika nchini humo.