TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MAWAZIRI WA AFRICA - FEDHA NA JINSIA

anzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-Afritac East), utakaofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 15 hadi 17, Novemba, 2023. Wakizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima, wameeleza kuwa Mkutano huo unalenga kujadili kuhusu namna yakuwawezesha wanawake na wasichana kiuchumi na kijamii kupitia ufadhili wa usawa wa kijinsia. Nchi zinazotarajiwa kushiriki Mkutano huo ni Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda.