TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA HISPANIA KUKUZA UCHUMI

Serikali imeeleza kuwa iko tayari kushirikiana na Hispania katika maeneo ya kipaumbele ikiwemo kukuza uchumi endelevu, ujenzi wa miundombinu, mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na kuendeleza rasilimali watu, kwa lengo la kuchochea maendeleo jumuishi nchini. Hayo yalielezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Hispania chini, Mhe. Paloma Serra Robles, aliyefika kwa ajili kujitambulisha na kuwasilisha masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Hispania, katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, Dodoma.