TANZANIA, DENMARK KUBADILISHANA UTALAAMU KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO
Tanzania na Denmark zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kutekeleza program ya maboresho ya mifumo ya kodi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaabani kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kodi wa Denmark, Mhe. Jeppe Bruus, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya.