SWEDEN YAONESHA NIA YA UWEKEZAJI KWENYE BIASHARA NCHINI
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Sweden kwa misaada mbalimbali iliyoweka alama chanya katika maendeleo ya kiuchumi katika sekta ya nishati, elimu na masuala ya demokrasia.
Amesema hayo jijini Dodoma, wakati wa mkutano wake na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ulioangazia ushirikiano wa maendeleo kati ya nchi hizo mbili.