SWEDEN KUSAIDIA UJENZI WA SGR

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na Biashara ya Nje wa Sweden, Mhe. Diana Janse, jijini Dodoma, ambapo Naibu Waziri huyo, amemweleza Mhe. Dkt. Nchemba kuwa, nchi yake inaandaa Mkakati Mpya wa Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili unaolenga kuongeza ushirikiano katika Nyanja za kiuchumi na kibiashara. Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Nchemba aliishukuru Sweden kwa kusaidia maendeleo ya nchi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika sekta za nishati, elimu, maendeleo ya Jamii kupitia Mfuko wa TASAF pamoja na mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa SGR, kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida ambacho ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 96.