SHIRIKA LA BIMA LA CHINA’ (SINOSURE) LAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Shirika la Bima la China - (CHINA EXPORT AND CREDIT INSURANCE CORPORATION (SINOSURE), imeahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania ambao umekuwepo kwa muda mrefu kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo ya watu. Ahadi hiyo Imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Zha Weimin alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.