SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUIMARISHA USHIRIKIANO KUFANIKISHA TATHMINI YA UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU NA UFADHILI WA UGAIDI MWAKA 2028

Serikali imezitaka taasisi zote zinazohusika na mapambano dhidi ya utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi kuimarisha ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri zaidi katika Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa kufanyika mwaka 2028. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua mafunzo ya maandalizi ya tathmini hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro, chini ya Kundi la Afrika Mashariki na Kusini la Kupambana na Utakatishaji Fedha Haramu (ESAAMLG).