SERIKALI YAZIPOKEA CHANGAMOTO ZA WENYE VIWANDA; YAAHIDI MAZINGIRA BORA YA KIBIASHARA KATIKA BAJETI IJAYO.
Serikali imewahakikishia wamiliki na wadau wa viwanda nchini kuwa inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara, huku ikibainisha kuwa mapendekezo yaliyowasilishwa na wadau hao yanafanyiwa kazi kwa kina kuelekea kipindi cha Bunge la Bajeti.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), iliyowakutanisha viongozi wa Serikali na wadau wa viwanda kwa lengo la kutathmini, kuoanisha mikakati, na kutatua changamoto zinazozuia kasi ya ukuaji wa sekta hiyo, iliyofanyika xkatika ukumbi wa hotel ya Four Point, jijini Dar es Salaam.
