SERIKALI YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA UKOMO WA BAJETI 2024/2025

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha na Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.39. Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu.