SERIKALI YASISITIZA UTAALAMU NA UBUNIFU KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufanisi, uwazi na tija katika matumizi ya fedha za umma. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua Kongamano la 16 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lenye kaulimbiu ya “Kukuza Wataalam wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi watakaojiimarisha katika Ujuzi wa Uongozi na Ubunifu” lililoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.