SERIKALI YASISITIZA NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI.
Serikali imewaagiza wataalamu wanaosimamia mipango na bajeti katika wizara na taasisi mbalimbali nchini kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma ili kuboresha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na Sekretarieti za mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
