SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA PPP KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) Serikali inatambua na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP) kama njia muhimu ya kuongeza rasilimali Fedha na kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini. Mhe. Balozi Omar alisema hayo wakati akifungua rasmi Kozi Fupi ya Kumi na Saba ya Viongozi (Capstone 17) yanayotolewa na Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kilichoko Kunduchi, jijini Dar es Salaam.