SERIKALI YAKIAGIZA CHUO CHA MIPANGO KUWA KITOVU CHA MAARIFA NA UBUNIFU KUELEKEA DIRA 2050
Serikali ameliagiza Baraza la 14 la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuhakikisha Chuo hicho kinakuwa kitovu cha maarifa, tafiti na utaalamu utakaosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi na utekelezaji wa Dira 2050.
Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) katika uzinduzi rasmi wa Baraza hilo.
Mhe. Luswetula alisema Chuo hicho kina nafasi muhimu katika kuandaa wataalamu wenye ujuzi wa kupanga na kusimamia maendeleo, hivyo kinapaswa kuhakikisha programu zake za mafunzo, tafiti na ubunifu zinaendana na mahitaji ya uchumi wa sasa na wa baadaye.
