SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI KATIKA SEKTA ZA MIUNDOMBINU, NISHATI NA KILIMO

Serikali ya Tanzania imewakaribisha wawekezaji kutoka Uturuki kuwekeza katika sekta za kimkakati zikiwemo miundombinu, nishati na kilimo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuharakisha maendeleo ya uchumi na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Wito huo umetolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati alipokutana na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Bekir Gezer, akiambatana na ujumbe kutoka Benki ya EXIM ya Uturuki, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.