SERIKALI YAITAKA NBAA KUBUNI MITAALA KUENDANA NA MAPINDUZI YA AKILI UNDE.

Serikali imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kuharakisha maboresho ya mitaala na mafunzo ya uhasibu ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia, hususan matumizi ya akili unde (AI), kwa kuwa baadhi ya kazi zinazofanywa na wahasibu hivi sasa zinaweza kubadilika au kutoweka kutokana na mapinduzi hayo ya kiteknolojia. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), wakati akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika Mahafali ya 49 ya NBAA yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha APC-Mbweni, jijini Dar es Salaam.