SERIKALI YAHITIMISHA KWA MAFANIKIO ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU YA FEDHA MKOANI MTWARA

Serikali kupitia Wizara ya Fedha imehitimisha mafunzo ya elimu ya fedha Mkoani Mtwara ikiwa ni juhudi za kuimarisha uelewa wa masuala ya kifedha miongoni mwa wananchi. Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji na Dhamana, wametoa mafunzo hayo kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara ambayo yalihusisha washiriki kutoka sekta mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, wavuvi, makundi maalum na vijana kutoka katika Wilaya zote za Mkoa huo kuanzia tarehe 22 Julai,2024 na kuhitimishwa tarehe 30 Julai, 2024.