SERIKALI YAHIMIZA WANANCHI KUPATA ELIMU YA FEDHA
Katika jitihada za kuimarisha ustawi wa wananchi na kukuza uchumi wa Taifa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza katika elimu ya fedha kwa kuandaa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika mkoani Tanga, yakilenga kuwajengea wananchi nidhamu na uelewa wa matumizi sahihi ya huduma za kifedha.
Maadhimisho hayo, yanayoandaliwa na Wizara ya Fedha, yatafanyika katika Viwanja vya Usagara jijini Tanga kuanzia Januari 19 hadi 26, 2026, na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb).
