SERIKALI YAENDESHA WARSHA KUJENGA USHIRIKIANO NA WASHIRIKA WA MAENDELEO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendesha mafunzo ya siku moja kwa Washirika wapya wa Maendeleo na Wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyojikita katika kuimarisha uelewa wa taratibu, sera, na mikakati ya maendeleo ya nchi pamoja na kushirikiana katika utekelezaji wa Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF) katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Fedha wakati akifungua warsha hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam, Kamishina, Idara ya Fedha za Nje, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Zanzibar Bw. Yussuf Ibrahim Yussuf alisema kuwa dhamira ya warsha hiyo ni kuhakikisha serikali inaweka ushirikiano madhubuti na Washirika wa Maendeleo.