SERIKALI YAELEZA DHAMIRA YAKE KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI.

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), katika Mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. Alieleza kuwa, Serikari inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia Sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za kuendeleza vipaji vyao na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.