SERIKALI YAAGIZA SEKTA ZOTE KUTUMIA WANUNUZI WENYE SIFA
Serikali imewaagiza waajiri wa Sekta zote nchini kuhakikisha wataalam wanaofanya shughuli za ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa sitahiki kama ilivyoainishwa kwenye Sheria Na. 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), pamoja na miongozo inayotolewa.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.