SERIKALI YAAGIZA ELIMU YA FEDHA IWE ENDELEVU

Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha wameagizwa kuhakikisha Programu ya Elimu ya Fedha kwa Umma inakuwa endelevu ili kuongeza wigo wa uelewa na utumiaji wa huduma za fedha. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella , wakati wa kufunga Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.