SERIKALI KUWEZESHA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUPATA MAKAZI BORA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde (Mb), amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za fedha likiwemo Shirika la Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) ili kuiwezesha sekta ya fedha kupata mikopo yenye gharama nafuu, hatua itakayosaidia jamii ya kipato cha chini kumiliki makazi bora. Mhe. Munde amesema hayo Jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akizindua rasmi huduma ya mikopo midogo ya makazi jijini Dar es Salaam, iliyoanzishwa na Shirika la Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) kwa kushirikiana na Shirika la Habitat for Humanity International, iliyokusudiwa kuziwezesha taasisi za fedha kupata ukwasi wa shilingi bilioni 30, ili ziweze kutoa mikopo midogo ya nyumba, kwa wananchi wenye kipato cha chini kwa lengo la kuwawezesha kumiliki makazi bora.