SERIKALI KUU YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 27.4 KUTOKA BENKI YA CRDB

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Serikali imepokea gawio la kiasi cha shilingi bilioni 27.4 kutoka Benki ya CRDB kutokana na Serikali Kuu kumiliki asilimia 21 ya Benki hiyo kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja na Serikali ya Denmark (DIF) Hayo yamesemwa jijini Dodoma kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati wa hafla ya Benki ya CRDB kuikabidhi gawio la mwaka 2023.