SERIKALI KUBORESHA NA KUONGEZA IDADI YA VYUO VIKUU NA VYA KATI NCHINI.

Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Vyuo Vikuu na vya Kati na kuongeza idadi ya vyuo hivyo katika mikoa yote ili wananchi wapate fursa zaidi ya kujiendeleza kimasomo na kupata elimu ya juu. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, katika Mahafali ya Hamsini na Moja ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), yaliyofanyika katika Ukumbi wa The Dimond Jubilee Hall, alisema Serikali imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kuboresha elimu ili kukuza uchumi.