SERIKALI IMEPIGA HATUA KIUCHUMI, KIDEMOKRASIA NA UTAWALA BORA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Tanzania itaendelea kuwekeza fedha kwenye sekta za uzalishaji, kudumisha demokrasia na utawala bora ili kukuza uchumi wa nchi na ustawi wa jamii. Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC), jijini Dodoma waliopo nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya masuala mbalimbali baada ya Shirika hilo kuichagua Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazonufaika na ruzuku zinazolenga kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji wa uchumi, demokrasia, utawala bora na maendeleo ya rasilimali watu.