SERA YA TAIFA YA UGAVI YAZINDULIWA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA NA UPENDELEO.

Serikali imezindua Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya Mwaka 2025, inayolenga kufanya mageuzi makubwa katika mnyororo wa thamani, huku ikitajwa kuwa mwarobaini wa kudhibiti mianya ya upotevu wa rasilimali na kukuza ushiriki wa wazalishaji wa ndani katika uchumi wa Taifa. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akizindua Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya Mwaka 2025, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.